TAMASHA LA MBIO NDEFU LA KIHISTORIA LA BAGAMOYO KUFANYIKA TAREHE 24 JULY
2016
Ndugu
waandishi wa habari,
UTANGULIZI
Tamasha
La Bagamoyo Historical Marathon
litafanyika kwa mara ya tatu (3) siku ya Jumapili, tarehe 24 July 2016 kuanzia
saa 12:00 asubuhi.
Ndugu
waandishi wa habari, Tamasha la pili la Bagamoyo Historical Marathon lilifanyika
kwa mara ya kwanza na kwa mafanikio mjini Bagamoyo tarehe 14 Juni 2015 ambapo lilihudhuriwa
na takriban watu 2000. Tunawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya mafanikio yale.
Karibuni tena na tunaomba ushirikiano wenu kufanikisha na hili pia.
Maudhui yetu mwaka huu ni “ANZA KUKIMBIA, UJIKINGE NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA” yaani “PREVENT NON-COMMUNICABLE DISEASES, START RUNNING”.
Nia na Madhumuni:
· KUHAMASISHA AFYA BORA– kutokana na ongezeko kubwa la matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukizwa (Non-Communicable Diseases-NCDs) , Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbali mbali inasisitiza mazoezi hasa kutembea, mchaka-mchaka (jogging) na kukimbia kama njia kuu ya kudumisha afya na kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, shinikizo la damu n.k.
· KUKUZA UTALII – kama inavyofahamika Bagamoyo ndiyo mji mkongwe kuliko miji yote nchini Tanzania ambao umepitishwa na UNESCO kuwa eneo la saba lenye uhifadhi wa historia ya kale (Seventh World Heritage Site).
· KUCHANGIA MAENDELEO KIUCHUMI – kwa kuwa matarajio yetu ni kuwa na wageni wengi kwa tukio hili katika mji wa Bagamoyo tunatumaini kuwa tukio hili litaongeza shughuli za kibiashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo hivyo kuboresha uchumi wa mji huu.
· KUENDELEZA RIADHA TANZANIA
Na nia ya mwisho, japo ndio kuu hasa, ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji vya mbio ndefu.
Mbio hizi zinatarajia kushirikisha makundi ya mbali mbali ya watu kama ifuatavyo:-
Wakimbiaji wataaluma(professional athletes)
Kilomita 21.1 Umri wa miaka 14 na kuendelea.
Wakimbiaji wengine (casual runners)
KM 10 Umri wa miaka 14 na kuendelea
KM 5 Family Fun Run.
Tamasha hili litajumuisha mbio zifuatazo:-
Mbio ndefu za 21.1 km (Half Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:30 asubuhi (6:30AM sharp) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia (Mangesani Road) na baadaye, kupitia Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam na kugeuzia maeneo ya Kiromo.
Mbio ndefu za 10.5 km (Quarter Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:45 asubuhi (6:45AM) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road, katikati ya mji na kisha kuchukua Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam mpaka makutano ya Barabara ya Msata. Kisha watachukua uelekeo wa kuelekea Msata takribani kilomita nne (4) ambapo watageuza kurejea uwanja wa shule ya Mbaruku.
Mbio za kujifurahisha (Fun Run) - Mbio hizi zinatarajiwa kuanza saa 01:00 pale uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road na kuelekea upande wa mahoteli ya kitalii mpaka kufika kituo cha zimamoto ambapo washiriki watageuza kurudi uwanja wa Mbaruku.
event website: www.bagamoyomarathon.co.tz
Hotline: +255 655 55 00 66
Hotline: +255 655 55 00 66
-->