Maudhui
yetu mwaka huu ni “ANZA KUKIMBIA,
UJIKINGE NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA” yaani “PREVENT NON-COMMUNICABLE DISEASES, START RUNNING”. Hivyo uzinduzi wa mwaka huu ulifanywa na
Mwakilishi wa Waziri wa Afya tarehe 19 Machi 2015 mjini Bagamoyo. Pia uzinduzi
ulipata uwakilishi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo na pia Chama cha Riadha
Tanzania.
Nia na Madhumuni:
· KUHAMASISHA
AFYA BORA– kutokana na ongezeko kubwa
la matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukizwa (Non-Communicable Diseases-NCDs) ,
Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbali
mbali inasisitiza mazoezi hasa kutembea, mchaka-mchaka (jogging) na kukimbia kama njia kuu ya kudumisha afya na kinga
dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, shinikizo la damu n.k.
Mbio hizi zitahamasisha ufanyaji wa mazoezi hasa yale ya kukimbia na hivyo
kusaidia kupunguza matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza.
· KUKUZA UTALII – kama inavyofahamika Bagamoyo ndiyo mji mkongwe kuliko miji yote nchini Tanzania ambao umepitishwa na UNESCO kuwa eneo la saba lenye uhifadhi wa historia ya kale (Seventh World Heritage Site). Mji huu ulikuwa moja ya soko kuu la watumwa katika Afrika mashariki na kati, hivyo mbio hizi zitasaidia kuutangaza, kuhamasisha na kukuza utalii katika mji huu muhimu kihistoria nchini na hivyo kuchangia kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.
·KUCHANGIA MAENDELEO KIUCHUMI – kwa kuwa matarajio yetu ni kuwa na wageni wengi kwa tukio hili katika mji wa Bagamoyo tunatumaini kuwa tukio hili litaongeza shughuli za kibiashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo hivyo kuboresha uchumi wa mji huu.
· KUENDELEZA RIADHA TANZANIA
Na nia ya mwisho, japo ndio kuu hasa, ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji vya mbio ndefu na baadaye kujenga kambi itakayowawezesha kuwajenga kinidhamu ili waweze kushiriki na kushinda mbio ndefu maarufu duniani siku za usoni. Tunaamini katika maandalizi sahihi ya washiriki ili kurejesha vyema heshima ya Tanzania katika mchezo wa riadha.
Mbio hizi zinatarajia kushirikisha makundi ya mbali mbali ya watu kama ifuatavyo:-
Wakimbiaji wataaluma(professional athletes)
Kilomita 21.1 Umri wa miaka 14 na kuendelea.
Wakimbiaji wengine (casual runners)
KM 10 Umri wa miaka 14 na kuendelea
KM 5 Family Fun Run.
Tamasha hili litajumuisha mbio zifuatazo:-
Mbio ndefu za 21.1 km (Half Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:30 asubuhi (6:30AM sharp) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia (Mangesani Road) na baadaye, kupitia Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam na kugeuzia maeneo ya Kiromo.
Mbio ndefu za 10.5 km (Quarter Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:45 asubuhi (6:45AM) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road, katikati ya mji na kisha kuchukua Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam mpaka makutano ya Barabara ya Msata. Kisha watachukua uelekeo wa kuelekea Msata takribani kilomita nne (4) ambapo watageuza kurejea uwanja wa shule ya Mbaruku.
Mbio za kujifurahisha (Fun Run) - Mbio hizi zinatarajiwa kuanza saa 01:00 pale uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road na kuelekea upande wa mahoteli ya kitalii mpaka kufika kituo cha zimamoto ambapo washiriki watageuza kurudi uwanja wa Mbaruku.
Kutembelea sehemu za Kihistoria.
Hii ni nafasi nzuri sana kwa wale watakaweza kufika Bagamoyo siku moja kabla (Jumamosi ya tarehe 13 Juni) na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria Bagamoyo, kama, Kaole ruins, Kanisa la Mwanzo Africa Mashariki, nk.
Weekend gateaway
Bagamoyo kuna hotel nzuri sana za ufukweni, hivo tunawahimiza hasa watu wa Dar es salaam kufika na ku ‘refresh’ baada ya shughuli za kila siku kwenye jiji letu hili la Dar es salaam. Tungependa sehemu kubwa ya jiji ihamie Bagamoyo wikiendi ya tarehe 14. Mazungumzo yanaendelea na hotel mbali mbali za Bagamoyo ili kupata malazi kwa bei za punguzo.
BURUDANI
Mbdio hizi
zinadhaminiwa na Coca Cola, E- Fm; Tanzania Standard News Papers, Azam Media,
Oceanic Bay Hotel & Resort , Inoga Hotel na Watu Binafsi. Tupo mbioni pia
kukamilisha udhamini kutoka kwa wadau wengine wa Michezo na Afya. Tunaomba
ushirikiano kutoka wadau wa michezo na pia watu wote wenye mapenzi mema na mchezo
wa riadha ili kuboresha azma yetu. Maelezo zaidi yanapatika kwenye website yetu
www.bagamoyomarathon.co.tz
ZAWADI
Ndugu Waandishi
wa Habari, Tunatarajia kuwa na zawadi nono na kwa washiriki wengi, kama
ifuatavyo:-
21.1 km Half Marathon
|
10.5 km Half Marathon
|
||||
Gents
|
Ladies
|
Gents
|
Ladies
|
||
Mshindi 1
|
500,000
|
500,000
|
100,000
|
100,000
|
|
Mshindi 2
|
400,000
|
400,000
|
80,000
|
80,000
|
|
Mshindi 3
|
300,000
|
300,000
|
50,000
|
50,000
|
|
Mshindi 4
|
200,000
|
200,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 5
|
150,000
|
150,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 6
|
100,000
|
100,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 7
|
80,000
|
80,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 8
|
50,000
|
50,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 9
|
50,000
|
50,000
|
40,000
|
40,000
|
|
Mshindi 10
|
50,000
|
50,000
|
40,000
|
40,000
|
|
1,880,000
|
1,880,000
|
510,000
|
510,000
|
UANDIKISHWAJI
Ndugu
waandishi wa Habari ,
Uandikishwaji
utaanza rasmi siku ya Jumatano tarehe 03 Juni
2014, katika maeneo yafuatayo:-
· Tunatarajia kuwa na Vituo mbalimbali
jijini na kwa kuanzia tutakuwa Quality Centre na Msasani Mall kwa kuanzia. Vituo
vingine tutaendelea kufahamishana kadiri tunavyovipata.
-->
No comments:
Post a Comment