TAARIFA
YA MKURUGENZI MKUU BW. JOSEPH B. MASIKITIKO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA
VIWANGO BARANI AFRIKA KATIKA NGAZI YA KITAIFA, ILIYOTOLEWA TAREHE 27 JANUARI,
2016
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni
Shirika lenye dhamana ya kuandaa Viwango vya kitaifa na kudhibiti ubora wa
bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazotoka nje ya nchi ili kumlinda
mlaji na mtumiaji wa bidhaa hizo.
SGS Representative giving a word during press meeting Mr. Hemed |
Katika kufanikisha hilo, TBS ni mwanachama
wa umoja wa waandaaji wa Viwango barani
Afrika (ARSO), na maadhimisho ya siku ya Viwango katika ngazi ya bara la Afrika
yanafanyika kila mwaka kati ya mwezi
Januari na Februari. Kauli mbiu ya mwaka
huu ni Mchango wa Viwango Katika Kuwawezesha na
Kuwaendeleza Wanawake yaani “How Standards Contribute to Women’s Empowerment and
Development”
Tanzania kupitia TBS itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa Viwango barani Afrika mwaka huu ambao utaambatana na shughuli za maonyesho ya bidhaa za kitanzania yaani ‘made in Tanzania products’.
TBS kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) wameandaa maonyesho ya bidhaa za kitanzania ikiwa ni sambamba na maadhimisho ya siku ya Viwango Afrika (ARSO) katika ngazi ya kitaifa, yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Februari 2016 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Ushiriki wa mwaka huu utatoa fursa kwa makampuni mbalimbali kuonyesha bidhaa zao na kushiriki katika kupata bidhaa bora za Ki-Tanzania ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya bidhaa katika ngazi ya bara la Afrika ili kupata “Made in Africa”.
Hii itafungua milango kwa bidhaa za Ki-tanzania kuingia katika masoko ya nje ya nchi pamoja na uhamasishaji kwa jamii ya Tanzania kununua bidhaa za Ki-Tanzania yaani bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Pia lengo kuu la maadhimimisho haya ni kuwakutanisha wazalishaji wa viwandani, wafanyabiashara, taasisi za Serikali pamoja na sekta binafsi na kuzungumzia juu ya mchango wa Viwango katika kukuza biashara ndani na nje ya nchi, kupanua mitaji, kuongeza ajira na kuboresha hali na maisha ya watanzania kwa kutumia bidhaa bora na salama.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2017 umepangwa na umoja wa Afrika kama mwaka wa uimarishaji wa miundombinu ya ubora barani Afrika na hii imefikiwa na kikao cha wakuu wa nchi za Afrika kilichofanyika Adis Ababa, Ethiopia mwaka 2012 na kupanua biashara barani Afrika kwa asilimia 25 hadi 30. Hii ni fursa muhimu kwa wazalishaji wa ndani kutumia nafasi hii adhimu katika kupanua masoko ya bidhaa zao.
Katika maonyesho hayo tunategemea mambo yafuatayo;
· Wazalishaji wa ndani kuonyesha uwezo wao katika kutumia Viwango na kuzalisha bidhaa bora na salama,
· Wajasiriamali kujifunza na kuzitambua fursa zilizopo katika utumiaji wa Viwango vya bidhaa katika kupata masoko, kuchochea uwekezaji pamoja na kupata mitaji,
· Kushindanisha bidhaa kutoka kwa wazalishaji wakubwa, wa kati na wadogo ili kupata bidhaa 50 au zaidi zitakazoshindanishwa wakati wa Mkutano mkuu wa ARSO mwezi Juni mwaka huu utakaofanyika jijini Arusha ambapo nchi zipatazo 35 zinatarajiwa kuhudhuria.
· Bidhaa zitakazoshindanishwa wakati wa mkutano huo zitapata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya ubora wa bidhaa yanayoandaliwa kila mwaka katika nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC awards. Hii itafanya bidhaa za kitanzania kuingia kwa wingi kwenye soko la jumuiya ya SADC.
· Bidhaa 20 zitakazochaguliwa mwezi Juni zitashindanishwa kwenye mashindano ya bara la Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Misri mwakani (2017).
Stall preparations |
Maadhimisho haya yataleta chachu kubwa
katika haya yafuatayo;
·
Kuchochea maendeleo
kwa kuongeza matumizi ya Viwango katika kutengeneza bidhaa na kutoa
huduma mbalimbali nchini.
·
Kuongeza matumizi ya Viwango katika kutoa alama ya ubora.
·
Kuzitambua alama za ubora na faida zake kwa wafanyabiashara,
wazalishaji na watumiaji wa bidhaa.
·
Kuhimiza matumizi ya bidhaa za ndani zenye alama ya ubora.
·
Kujenga utangamano wa kibiashara ndani na nje ya nchi.
·
Kuvutia wawekezaji na wafanya biashara kununua bidhaa za
kitanzania zenye nembo ya ubora.
·
Kuongeza soko la nje.
Hivyo, tunawakaribisha kushiriki na
kujifunza kuhusu Viwango pamoja na shughuli mbalimbali za kukuza biashara yako
ndani na nje ya taifa letu katika maadhimisho hayo.
Aksanteni kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment